KENYA-SOMALIA

Jeshi la Kenya lawauawa wapiganaji 15 wa Al Shabab nchini Somalia

Wapiganaji wa Al Shabab nchini Somalia
Wapiganaji wa Al Shabab nchini Somalia Wikipedia

Jeshi la Kenya linasema limewauwa wapiganaji 15 wa Al Shabab nchini Somalia.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Jeshi hilo Kanali Joseph Owuoth amesema wapiganaji hao waliuawa katika eneo la Catamaa katika jimbo la Gedo walipovamiwa na jeshi hilo.

Jeshi la Kenya ambalo linapambana na Al Shabab chini ya jeshi la Umoja wa Afrika AMISOM, limekuwa likisema linafanikiwa kuwauawa wapiganaji wengi wa kundi hilo na kuharibu kambi zao Kusini mwa nchi hiyo.

Kundi la Al Shabab nalo limeendelea kuwa hatari kwa usalama wa wanajeshi baada ya kuwahi kutekeleza mashambulizi katika kambi za wanajeshi hao na kufanikiwa kuwauwa wanajeshi kadhaa hivi karibuni ikiwa katika kambi ya Kulbiyow mwezi Januari.

Serikali ya Kenya ambayo inapambana na kundi Al Shabab chini ya mwavuli wa jeshi la Umoja wa Afrika AMISOM.

Nchi hiyo, ilituma kikosi chake mwaka 2011 nchini Somalia  kupambana na magaidi hao waliokuwa wameanza kuhatarisha usalama wa nchi yake na  kuwateka watalii katika eneo la mpakani.