UN yatoa wito wa kusitisha mapigano Sudan Kusini
Imechapishwa:
Umoja wa Mataifa hapo jana umetoa wito wa kusitisha mapigano nchini Sudan Kusini baada ya serikali kuzindua mashambulizi mapya mapema juma hili.
Siku ya Jumatano, Vikosi vinavyounga mkono serikali ya Sudan Kusini vililenga mji mmoja unaopatikana kaskazini mwa nchi na kusababisha raia kukosa makazi ambao kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa wanaweza kuwa wamekimbilia kwenye mpaka na Sudan.
Stephane Dujarric, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema katika taarifa kuwa wanaguswa na kuongezeka kwa vurugu na mteso ya raia kutokana na shambulizi la karibuni la vikosi vya serikali.
Aidha umoja wa mataifa umesema Zaidi ya watu 95,000 raia wa Sudan Kusini hadi sasa wameingia nchini Sudan kwa mwaka huu,huku maelfu wakiendelea kukimbia vita na njaa katika taifa hilo dogo zaidi duniani