UGANDA-MUSEVENI-USALAMA

Museveni akiri kuwa ni dikteta mzuri

Yoweri Museveni, rais wa Uganda akihojiwa na al-Jazeera.
Yoweri Museveni, rais wa Uganda akihojiwa na al-Jazeera. Capture d'écran al-Jazeera

Raia nchini Uganda wamekuwa wameonekana kukerwa na mahojiano ya hivi karibuni ya rais yoweri Kaguta Museveni na shirika la habari la Aljazeera ambapo alizungumzia maswala kadhaa, ikiwa ni pamoja na udikteta unaoendelea nchini Uganda.

Matangazo ya kibiashara

Raia nchini Uganda wamekua wakisambaza mahojiano hayo katika mitandao ya kijamii, na kusema kuwa rais Museveni ametoa mbaya sana ya kusikitisha.

Katika mahojiano hayo, rais Museveni amesema kipindi chake cha miongo mitatu kama rais wa Uganda ni sahihi na anaendelea kupendwa na wananchi wa Uganda.

Akiulizwa kuhusu kwanini watu wengi wanamuita dikteta, rais Museveni kwanza aliwashutumu watu hao, akisema kuwa huenda amekuwa dikteta mzuri kwa sababu amekuwa akichaguliwa na wananchi mara tano.

Bw Museveni aliulizwa kuhusu kufungwa kwa mwanaharakati Stella Nyanzi ambaye anazuiliwa kwa kumuita, ''makalio" akisema kuwa hana haki ya kuwatusi wengine.

Rais Yoweri Museveni ni miongoni mwa maris wanaptawala nchi zao kwa miaka mingi.