TANZANIA-AJALI

Wanafunzi zaidi ya 30 nchini Tanzania wapoteza maisha kutokana na ajali ya barabarani

Basi la wanafunzi lililopata Kaskazini mwa Tanzania Mei 6 2017
Basi la wanafunzi lililopata Kaskazini mwa Tanzania Mei 6 2017 Wikipedia

Wanafunzi na walimu wa shule ya msingi 35 wameaga dunia Kaskazini mwa nchi ya  Tanzania siku ya Jumamosi baada ya gari walilokuwa wanasafiria kutumbukia mtoni.

Matangazo ya kibiashara

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo ameiambia RFI Kiswahili kuwa ajali hiyo ilitokea Jumamosi asubuhi wakati basi dogo likiwasafirisha wanafunzi kutoka mjini Arusha kwenda Karatu kwa shughuli za masomo.

Mkumbo ameeleza kuwa kwa jumla wanafunzi waliofariki duniani ni 32, huku wawili wakiwa walimu pamoja na dereva wa basi hilo.

Aidha, amesema kuwa hadi sasa haijafahamika chanzo cha ajali hiyo lakini uchunguzi bado unaendelea.

"Bado hatujafahamu kiuhalisia kilichosababisha ajali hiyo lakini wakati ikitokea, kulikuwa na mvua iliyokuwa inanyesha,"

"Hatufahamu ikiwa mvua ndio iliyosababisha dereva kupoteza mwelekeo au kama kulikuwa na tatizo lingine la gari," alisema Kamanda Mkumbo.

CHARLES MKUMBO KAMANDA WA POLISI MKOANI NCHINI TANZANIA ARUSHA.aif 16.42

Imebainika kuwa wanafunzi waliopoteza maisha walikuwa ni wa darasa la saba kutoka shule ya kibinafsi ya LackVicent yenye makao yake mjini Arusha.

Rais John Pombe Magufuli amesema amesikitishwa sana na mkasa huu na kutuma salamu za pole kwa jamaa ndugu na marafiki.