Uchaguzi ndani ya vyama vya siasa nchini Kenya umemalizika. Wagombea wa nyadhifa mbalimbali wamepatikana, lakini ni zoezi ambalo limedaiwa kukumbwa na ufisadi na hata baadhi ya wanasiasa kutapelewa. Hali hii pia imesababisha kuwepo kwa wagombea binafsi zaidi ya elfu mbili. Tunajadili zoezi hili kwa kina.