SUDAN KUSINI

Jenerali Paul Malong asema hana nia ya kuanzisha uasi dhidi ya rais Salva Kiir

Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi nchini Sudan Kusini Jeneralo Paul Malong
Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi nchini Sudan Kusini Jeneralo Paul Malong Yutube

Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi nchini Sudan Kusini Jenerali Paul Malong Awan aliyefutwa kazi wiki hii na rais Salva Kiir, amesema hana nia ya kuanzisha uasi dhidi ya serikali ya Juba.

Matangazo ya kibiashara

Jenerali Malon alitoa hakikisho hilo alipozungumza na raia wa nchi hiyo katika mji wa Yirol katika jimbo la Lakes.

Kumekuwa na wasiwasi jijini Juba kutokana na hatua ya Jenerali huyo kuondoka muda mfupi baada ya kufutwa kazi, kama ishara kuwa alikuwa anapanga uasi dhidi ya rais Kiir.

Ripoti zinasema kuwa haijafamika ni vipi Malong, alifanikiwa kuondoka jijini Juba hata kabla ya kukadhi Ofisi kwa Mkuu mpya wa Majeshi.

Aidha, inaelezwa kuwa hatua yake ya kutoa kauli yake wazi, ilikuja baada ya wito kutoka kwa washirika wake wa karibu ili kuondoa wasiwasi kuwa alikuwa na mpango dhidi ya uongozi wa Juba.

Malong amesema hajawahi kuwa muasi dhidi ya serikali au hata raia wa Sudan Kusini na hawezi kufanya hivyo.

Msemaji wa jeshi Kanali Santo Domic Chol amethibitisha kuondoka kwa Malong jijini Juba na kuthibitisha kuwa nia yoyote ya kuanzisha mapigano.

Sudan Kusini imeendelea kukosa amani tangu mwaka 2015 licha ya kutiwa saini kwa mkataba wa kisiasa jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kati ya rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar.