SUDAN KUSINI

Mku wa majeshi aliyefutwa kazi arejea Juba

Mkuu wa zamani wa majeshi ya Sudani Kusini Paul Malong
Mkuu wa zamani wa majeshi ya Sudani Kusini Paul Malong rfikiswahili/Ali Bilal

Mkuu wa majeshi aliyefutwa kazi hivi karibuni nchini Sudan Kusini Paul Malong, amerejea mjini Juba jana Jumamosi kwa madai kuwa ameombwa na mamlaka kurejea na kusisitiza kwamba kamwe hana nia yoyote ya kuasi.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuwasili mjini Juba Malong amewaambia waandishi wa habari kuwa kama angekuwa na nia ya kuasi angeasi akiwa hapo na kama angetaka kupambana angepambana hapo hapo Juba.

Malong ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa rais Salva Kiir alifutwa kazi siku ya Jumanne hatua ambayo ilielezwa kuwa hatua za kawaida lakini imeibua hofu na mapigano baina ya vikosi tiifu kwake na kwa rais Kiir.

Mwezi Februari maafisa kadhaa wa juu jeshini walijiuzulu,wakimtuhumu Malong kwa kuandaa vita ya kikabila dhidi ya raia wasio wa kabila la Dinka na kufanya maamuzi yasiyo na usawa kwa jamaa na rafiki zake.