UGANDA-MUSEVENI-HAKI

Rais Museveni aitaka polisi kutowatesa mahabusu

Yoweri Museveni, rais wa Uganda tangu mwaka 1986.
Yoweri Museveni, rais wa Uganda tangu mwaka 1986. Capture d'écran al-Jazeera

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameshutumu matumizi " yasiyohitajika na mabaya" kwa kuwatesa mahabusu au watu wanaoshikiliwa na polisi. Katika barua aliowatumia wakuu wa polisi na idara za usalama, Rais Yowezi Kaguta Museveni amewataka viongozi hao kutotumia nguvu na mateso kwa kuwahoji watu wanaoshikiliwa au wanaokamatwa.

Matangazo ya kibiashara

"Matumizi ya nguvu na mateso hayahitajiki na ni mabaya, na kama baadhi ya makundi wanavyodai kwenye vyombo vya habari, vitendo hivyo vilitekelezwa na vyombo vya usalama, kwa hiyo naomba hali hiyo isirudi kutokea, " rais Museveni ameandika, baada ya madai ya matumizi ya nguvu na mateso, vitendo vinavyotekelezwa na vikosi vya usalama ambavyo vimeongezeka katika wiki za hivi karibuni.

Vitendo vya mateso vinaweza kutumika kwa "mtu mbaya, lakini kwa mtu ambaye hana hatia, itakua si kumtendea haki, " amesema Bw Museveni, ambaye anaongoza Uganda kwa mkono wa chuma tangu mwaka 1986, kwenye barua iliyotolewa na ofisi ya rais.

"Kuna mtu ambaye anaweza kukubali kosa wakati ambapo hana hatia kutokana na mateso anayopata," na "mateso wakati mwingine si lazima kwani teknolojia ya kisasa ya polisi na ushahidi vinatosha kumtambua mhalifu, " Rais Museveni amebainisha.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) kwa muda mrefu lilithibitisha kwamba watu wanaozuliwa katika jela mbalimbali nchini Uganda walikabiliwa na mateso.

Katika ripoti iliyochapishwa mwaka 2009, iliyofahamika kwa jina la "Open Secret", HRW iliandika kuwa "mateso na kifungo cha muda mrefu jela vimebaki miongoni mwa ukiukaji wa haki za binadamu vinavyojirudi zaidi na ni miongoni mwa matatizo nchini Uganda."

Kwa kujibu barua ya Rais Museveni, Maria Burnett, mkurugenzi wa HRW barani Afrika ameelezea masikitiko yake kwenye Twitter "kwamba rais Museveni hajaomba uchunguzi ufanyike, wala watu ambao walipata mateso kutendewa haki."

Bw Museveni alijibu kwa madai ya hivi karibuni yaliyotolewa na watu kadhaa, ikiwa ni pamoja na Meya wa jiji la Kamwenge, Geoffrey Byamukama, magharibi mwa Uganda, anayeshikiliwa katika gereza la Nalufenya, kilomita 80 kutoka mji mkuu Kampala, ambaye alipigwa vikali na polisi hadi kupoteza fahamu na kupelekwa hospitalini.

Byamukama alisem akuwa alifanyiwa mateso na polisi iliyokua ikimuhoji kuhusu kuhusika kwake katika mauaji ya msemaji wa polisi wa Uganda, Andrew Kaweesi alieuawa mwezi Machi mwaka huu.