Burundi

Warundi 8000 washiriki mbio za amani

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ????

Zaidi ya watu elfu nane wameshiriki mbio za amani jana Jumamosi katika mitaa ya jiji la Bujumbura nchini Burundi, kwa lengo la kuionyesha dunia kwamba utawala amani nchini Burundi ulitumbukia katika mgogoro wa kisiasa kwa zaidi ya miaka miwili, kwa mujibu wa waandaaji.

Matangazo ya kibiashara

Mbio hizo, ambazo zimefanikiwa kutokana na kampeni imara ya kuhamasisha ndani ya nchi kwa wiki kadhaa, zimefanyika chini ya ulinzi wa polisi na jeshi na kushuhudiwa na rais Pierre Nkurunziza, kwa mujibu wa mashahidi na waandishi wa habari.

Burundi ilitumbukia katika mgogoro mnamo mwaka 2015 baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza kugombea awamu ya tatu madarakani, akikiuka kukiuka kikomo cha mihula miwili kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo na mpango wa amani wa mwaka 2006 uliomaliza vita ya zaidi ya muongo mmoja ya wenyewe kwa wenyewe.

Kuwania kwake muhula wa tatu na kushinda kumesababisha maandamano yaliyosababisha vifo vya takribani watu 500 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ingawa makundi ya misaada yanasema idadi ya kweli inaweza kuwa kubwa kama 2,500, huku zaidi ya warundi 420,000 wakilazimishwa kukimbilia uhamishoni.