BURUNDI-JAMII-NDOA

Watu wanaoishi katika ndoa zisizo halali watakiwa kuhalalisha ndoa zao Burundi

Pierre Nkurunziza awataka watu wanaoishi katika ndoa zisizo halali kuhalaliza ndoa zao.
Pierre Nkurunziza awataka watu wanaoishi katika ndoa zisizo halali kuhalaliza ndoa zao. REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimana

Baada ya rais wa Burundi kutoa onyo kwa watu wanaoishi katika ndoa zisizo halali kuwa wamehalalisha ndoa zao ifikapo mwisho wa mwaka huu, viongozi tawala sasa wamo mbioni kuwahamasisha na kuwashinikiza wahusika kufanya hivyo.

Matangazo ya kibiashara

Onyo hilo rais Pierre Nkurunziza amelitoa mnamo mei mosi mwaka huu ambapo amesema watu wanaoishi  kenye ndoa zisizo halali wawe wamefanya hivyo hadi mwisho wa mwaka. Kwa sasa viongozi tawala kwenye ngazi tofauti wamo mbioni kuwahamasisha raia haswa wahusika na kwa namna fulani kuwashinikiza kutekeleza onyo hilo kwa muda uliotolewa. Lakini baadhi ya wanaume ambao wako kwenye ndoa zisizo halali waliozungumza na idhaa hii wanaona hii ni kama kuwanyanyasa na kukiuka haki zao.

Msimamo huyo hata hivyo umekosolewa na mama huyu ambaye anasema hatua hii imekuja muda mwafaka kwani yeye amekuwa akimuomba mumewo wahalalishe ndoa yao lakini akakaidi.

Kutoka kujuwa zaidi nimemuuliza wakili Alexandre Ndikumana mchambuzi wa maswali ya sheria na haki za binadamui.

Kwa mujibu wa viongozi wale, ambao watakaidi kutekeleza hatua hii huenda wakapoteza haki ya kupata bure huduma ya matibabu kwa watoto wao na akinamama wanaojifungua.