KENYA-USAFIRI

Kenya kuzindua reli ya kisasa itakayosafiri Mombasa Nairobi

Askari polisi akitoa ulinzi wa mji wa Mombasa.
Askari polisi akitoa ulinzi wa mji wa Mombasa. AFP PHOTO/IVAN LIEMAN

Reli ya kisasa kutoka mjini Mombasa kwenda jijini Nairobi nchini Kenya inazinduliwa leo na rais Uhuru Kenyatta. Mradi huu umeigharimu serikali ya Kenya Dola za Marekani Bilioni 3.2, kwa msaada wa serikali ya China ambayo imesimamia ujenzi huo.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kufanyika kwa uzinduzi huo rais Kenyata atawaongoza viongozi wengine wa serikali kusafiria treni mpya katika reli hiyo inayotarajiwa kuchukua saa nne kufika jijini Nairobi.

Akizindua treni ya mizigo siku ya Jumanne jioni, Kenyatta alisema mradi huu ulilenga kuunda nafasi za kazi na kufanikisha uchumi wa Kenya.

Huu ni mradi wa Kihistoria kwa Wakenya, baada reli ya kwanza kujengwa zaidi ya miaka 100 iliyopita na wakoloni kutoka Uingereza.

Serikali nchini humo sasa inapanga kuendeleza ujenzi huo kuunganisha na nchi jirani ya Uganda.