BURUNDI-MAZUNGUMZO-USALAMA

Benjamin Mkapa: Natambua ugumu wa kazi yangu

Rais mstaafu wa Tanzania , ambaye pia ni mwezeshaji katika mgogoro wa kisiasa nchini Burundi, Benjamin Mkapa hapa ilikua mwaka 2010.
Rais mstaafu wa Tanzania , ambaye pia ni mwezeshaji katika mgogoro wa kisiasa nchini Burundi, Benjamin Mkapa hapa ilikua mwaka 2010. Wikimedia Commons/Copyright World Economic Forum

Wakati mazungumzo ya kisiasa ya warundi yakionekana kukwama, hotuba ya Mwezeshaji katika mazungumzo hayo, rais mstaafu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa alioitoa wakati wa mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mei 20 jijini Dar Es Salaam, imekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. 

Matangazo ya kibiashara

Katika nyaraka za hotuba hiyo zilzovuja, Benjamin Willima Mkapa ambae sio mara nyingi kuzungumzia shughuli zake katika mazungumzo ya Warundi, ametaja matatizo kadhaa anayo kabiliana nayo katika juhudi za kuwaleta pamoja wanasiasa wa Burundi.

Mkapa alisema sehemu moja ya upinzani hauna imani naye huku serikali ya Burundi ikiwa haina utashi wa kushiriki katika mazungumzo, hali ambayo inakwamisha mazungumzo hayo.

Vikao vya mazungumzo vimeandaliwa mara tatu mjini Arusha tangu kukabidhiwa kwa jukumu zito la kuwaleta pamoja wanasiasa wa Burundi, vikao ambavyo hata hivyo havikuzaa matunda yoyote hadi sasa.

Mwaka mmoja tangu uteuzi huo msuluhishi katika mzozo huo hajafaulu kuwaleta pamoja wadau wote wa mgogoro wa Burundi, badala yake amekuwa akikutana nao kwa nayakati tofauti huku akipokea mitazamo na mapendekezo tofauti kutoka kila upande, mitazamo ambayo imeonakena kuwa vigumu kuinganisha pamoja.

Seriali ya Burundi imeendelea kushikilia msimamo wake kwamba nchi ni tulivu, mazungumzo hayo lazima yafanyike nchini kati, wakati huo huo ikianzisha mchakato wa mabadiliko ya katiba, jambo ambalo linatupiliwa mbali na upinzani unaodai kuwa usalama ni mdogo huku watu wakitiwa nguvuni kiholela, matukio ya utesaji, unyanyasaji, na watu wanaotoweka katika mazingira tatanishi.

Neno msuguano limerejelewa mara nyingi katika hotuba hiyo ambapo serikali imeelezwa kuwajibika katika kusuasua kwa mazungumzo hayo. Mratibu anawataka viongozi wa serikali kuonyesha dhamira ya dhati ya kushiriki kwenye mazungumzo  na kuitaka ifute waranti ya kukamatwa kwa viongozi wa upinzani na wa mashirika ya kiraia, kuwaacha huru wafungwa na kukubali ushiriki wa makundi yanayo shikilia silaha.

Katika kutamatisha hotuba hiyo ilioonekana kuwa siri, Benjamin Mkapa ameeleza ofisi yake imeathirika mara kadhaa na uvujishwaji wa taarifa. Na kukumbusha kwamba baadhi ya nyaraka huwasilishwa kwa sekretarieti ya jumuiya ya Afrika mashariki.