UGANDA

Rais Museveni kulihotubia taifa, kugusia uchumi na usalama

Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni RFI

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anatarajiwa kulihotubia taifa kutoa ufafanuzi wa maswala mbalimbali yanayolikabili taifa hilo la Afrika Mashariki.

Matangazo ya kibiashara

Mwaka uliopita, rais Museveni aliahidi kupambana na ufisadi na kuahidi kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kuhusika.

Hotuba ya mwaka huu inakuja wakati huu nchi hiyo ikiendelea kupitia kupanda kwa gharama ya maisha, utovu wa usalama bila kusahau kuteshwa kwa washukiwa wa makosa mbalimbali katika rumande ya Nalufenya mjini Jinja.

Hili ni jukumu la kikatiba kwa rais Museveni ambaye ameongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30 sasa kuwaeleza wananchi wa nchi hiyo mwelekeo wa taifa hilo.

Hali ya Uchumi wa Uganda ni suala nyeti ambalo rais Museveni anatarajiwa kueleza ni wapi nchi hiyo ilipo kiuchumi na malengo ya serikali yake katika siku zijazo.

Museveni amekuwa katika mstari wa mbele kuhimiza uzalishaji wa bidhaa kwa wingi kwa lengo la kuuza nje ya nchi lakini kuunda nafasi za kazi.

Wabunge wa upinzani wanatarajiwa kukosoa hotuba ya rais Museveni ambaye wamekuwa wakimweleza kama dikteta.