KENYA-AFYA

Wauguzi nchini Kenya wagoma huku wagonjwa wakirejea nyumbani

Mgom wa Manesi nchini Kenya
Mgom wa Manesi nchini Kenya Reuters

Wauguzi katika hospitali za serikali nchini Kenya wanagoma kushinikiza serikali kutekelezwa mkataba wa kuongezewa mshahara, kama ilivyokubaliwa mwaka uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Mwezi Desemba mwaka 2016, Wauguzi wapatao 45,000 waligoma  lakini baadaye wakakubali kurudi kazini baada ya serikali kukubali kuwatekelezea mahitaji yao.

Mgomo huu ulianza siku ya Jumatatu katika hospitali kadhaa nchini humo, huku wagonjwa wakishindwa kupata huduma muhimu.

Sekta ya afya nchini Kenya inaongozwa na serikali za Kaunti, na mkutano wa hapo jana wa Baraza la Magavana uliafikiana kufanya kila kilicho ndani ya uwezo wao kuhakikisha kuwa mkataba huo unatekelezwa.

Madaktari nchini humo wanasema inawawia vigumu kufanya kazi zao bila wauguzi ambao ni kiungo muhimu katika sekta ya afya.

Daktari Austine Oduor Naibu mmoja wa viongozi wa Madaktari nchini humo amesema kazi zao zinatatizika sana kwa ukosefu wa wauguzi hospitalini.

“Tunashindwa kufanya kazi zetu kikamilifu kwa sababu wauguzi hawapo kazini,”

“Serikali haina budui bali kusikiliza kilio cha, kwa sababu bila mgomo  hakuna kinachoweza kufanyika,” Daktari Oduor ameimbia RFI.

Kaimu Naibu Mkuu wa chama cha Wauguzi nchini humo Morris Opetu amesisitiza kuwa maelfu ya wauguzi wataendelea kugoma hadi pale matakwa yao yatakapotekelezwa.

Mgomo huu mpya unakuja baada ya kukamilika kwa ule wa Madaktari uliodumu kwa zaidi ya miezi mitatu tangu mwezi Desemba mwaka uliopita.