SUDAN KUSINI-IGAD

Raisi Kiir wa Sudani Kusini kutohudhuria mkutano wa IGAD

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir The Japan Times

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amekataa mualiko wa wakuu wa nchi kutoka Jumuiya ya maendeleo ya nchi za IGAD unaofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa rais Kiir, Ateny Wek Ateny, amesema rais hana sababu nyingine ya kutohudhuria lakini ana mambo mengi ya kushughulikia nchini mwake.

Mkutano huu utakaong’oa nanga kuanzia Juni 12 utazungumzia hali tete ya usalama kwenye taifa la Sudan Kusini ambako maelfu ya raia wameikimbia nchi yao kutokana na vita.

Mkutano huo ambao utahudhuriwa na wakuu wa mataifa ya IGAD utaangazia hali ya kibinadamu inayoikabili sudani kusini na vikwazo vya utekelezwaji wa mkataba wa amani uliosainiwa August, 2015.

Maafisa kadhaa wa kijeshi na wa serikali wamethibitisha kuwa raisi Kiir alibadili mawazo yake akiwaza huenda viongozi wa kikanda watamshinikiza maamuzi yatakayopendelea upande wa waasi.