Habari RFI-Ki

Jamii yahamasishwa kuongeza uelewa juu ya watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi Albinism

Sauti 10:30
Jamii yahamasishwa kuwalinda walemavu wa ngozi
Jamii yahamasishwa kuwalinda walemavu wa ngozi ©Marie Frenchon/ONU

Dunia hii leo inaadhimisha siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu watu wenye Albinism.Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Amnesty International jumla ya watu 18 wenye albinism waliuawa nchini Malawi na watano walitekwa nyara toka mwezi Novemba mwaka 2014.Hata hivyo nchi kadhaa barani Afrika zimefanikiwa kudhibiti mauaji ya watu wenye Albinism wanaouawa kwa imani za kishirikina, vitendo ambayo wakati fulani vilikuwa vimekithiri kwenye ncui za Malawi, Tanzania na Msumbiji.Wanaharakati wanatumia siku hii kuzikumbusha Serikali na watu, umuhimu wa kuwakubali na kuwaona sehemu ya jamii.