KENYA-SOMALIA-AL SHABAB

Watu wanne wafariki dunia nchini Kenya kwa bomu la kutegwa barabarani

Picha ya moja ya ajali iliyotokana na shambulizi la Al Shabab nchini Somalia
Picha ya moja ya ajali iliyotokana na shambulizi la Al Shabab nchini Somalia rfikiswahili/Abuso

Watu wanne wameuawa na 11 kujeruhiwa baada ya basi la abiria kukanyaga bomu kando ya barabara kaskazini mwa Kenya jana Ijumaa, maafisa wamesema,hilo likiwa tukio la karibuni katika mfululizo wa mashambulizi ya aina hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo hakuna taarifa za kundi lolote kudai kuhusika na shambulizi hilo, lakini katika siku za hivi karibuni wanajihadi wa Al shabab wa nchini Somalia wamefanya mashambulizi ya mabomu ya kutegwa barabarani katika maeneo ya mpaka na kuua watu kadhaa, wengi wao wakiwa maafisa wa polisi.

Basi hilo lilikuwa linasafiri kutoka Lafey kwenda Elwak katika kaunti ya Mandera karibu na mpaka na Somalia.

Kenya inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu tarehe nane Agosti mwaka huu na suala la usalama limekuwa ajenda ya wanasiasa katika kampeni zao.