TANZANIA-USALAMA

Polisi wawili wa Tanzania wauawa kwa kupigwa risasi Kibiti

Rais John Magufuli amekuwa akitoa onyo kali kwa watu wanaotekeleza mauaji haya kuwa watachukuliwa hatua kali.
Rais John Magufuli amekuwa akitoa onyo kali kwa watu wanaotekeleza mauaji haya kuwa watachukuliwa hatua kali. Ikulu/Tanzania

Maafisa wawili wa usalama nchini Tanzania wamepigwa risasi na kuuawa katika Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani. Hali ya usalama imeendelea kutisha katika eneo hilo kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema mauaji hayo yalitekelezwa na watu wasiofahamika waliokuwa wamejihami kwa silaha na yalitokea karibu na eneo ambalo maafisa wengine 11 waliuawa mwezi Machi mwaka huu.

Vyombo vya Habari nchini Tanzania vinaripoti kuwa, lengo la mauaji hayo yalijafahamika.

Rais John Magufuli amekuwa akitoa onyo kali kwa watu wanaotekeleza mauaji haya kuwa watachukuliwa hatua kali.

Polisi mkoani Pwani imesem ainaendelea kuwasaka wahalifu, na kuwaonya watu wanaoshirikiana au kuwaficha wahalifu kwamba watachukuliwa hatua kali.