EU-UGANDA-WAKIMBIZI

EU kuipa Uganda Euro Milioni 85 kushughulikia wakimbizi

Antonio Guterres (kushoto) na mkurugenzi wa shirika la mpango wa Chakula Duniani (WFP), wakigawa chakula kwa wakimbizi katika mji wa Imvepi June 22.
Antonio Guterres (kushoto) na mkurugenzi wa shirika la mpango wa Chakula Duniani (WFP), wakigawa chakula kwa wakimbizi katika mji wa Imvepi June 22. RFI / Charlotte Cosset

Umoja wa Ulaya umeahidi kutoa Euro Milioni 85 kwa nchi ya Uganda kusaidia kuwashughulikia zaidi ya wakimbizi Milioni moja nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Ahadi hii imetolewa katika kongamano la siku mbili kuhusu wakimbizi linalomalizika leo jijini Kampala.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress amewatembelea wakimbizi wa Sudan Kusini Kaskazini mwa nchi hiyo na kutaka machafuko kumalizika katika taifa hilo ili kuepusha raia wa nchi hiyo kuyakimbia makwao.

Kupitia kongamano hili, Uganda inatarajiwa kupata Dila Bilioni 2 kusaidia kuwahifadhi wakimbizi hao.

Takwimu kutoka Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa Uganda kwa sasa inawapa hifadhi wakimbizi Milioni 1.2 kutoka Sudan Kusini , Burundi , Rwanda , Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lakini inaelemewa na gharama za kuwasaidia.