TANZANIA-ELIMU

Utata juu ya elimu ya wanafunzi wasichana kutorudi shule waibuka Tanzania

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. 12 Juni, 2017
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. 12 Juni, 2017 Ikulu/Tanzania

Wakati alipokua akizindua barabara mpya ilioko kati ya Bagamoyo na Msata, katika mkoa wa pwani siku ya Alhamisi wiki iliopita, rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, alitoa msimamo wake kuhusu suala la elimu kwa wanafunzi " wasichana waliojifungua". Matamshi yake yameibua mvutano mkubwa katika jamii nchini Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

"Wanafunzi wasichana wanaojifungua hawawezi kurudi kuhitimu masomo yao, kwa muda wowote ule nitakua bado rais wa Tanzania," alionya rais wa Tanzania. Msimamo huu wa rais John Pombe Magufuli inaonekana kufunga mjadala ulioanza tangu mwezi jana bungeni.

Hata ndani ya serikali, mawaziri wamegawanyika juu ya suala hilo: wale wanaotaka" haki sawa kwa wote iheshimishwe" dhidi ya wale wanaopendelea kukandamiza badala ya kuelimisha.

Ripoti ya shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch iliyochapishwa tarehe 16 Juni ilidai kuwa viongozi wa shule za Tanzania walikuwa wakifanya vipimo vya mimba kwa minajili ya kufukuza wanafunzi wajawazito, na hivyo kuwanyima haki yao ya elimu.

Kwa upande wa upande wa rais wa Tanzania wanafunzi waliofukuzwa shule kwa sababu ya ujauzito wanatakiwa kujielekeza nyumbani na kufanya kazi zitakazo wasaidia kimaisha kama vile biashara na kilimo. John Pombe Magufuli alisema kuwa wanaume wanaouwatunga mimba wasichana wa shule pia nao wanapaswa kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 30 na kuweka nguvu zao walizozitumia kuwatunga mimba wasichana hao kulima wakiwa jela. Sheria ya mwaka 2002 inaruhusu kufukuzwa kwawanafunzi wasichana wajawazito. Nakala hii ni misingi ya "kosa kwa maadili" na "ndoa".

Rais wa Tanzania amefutilia mbali madai ya mashirika yasio ya kiserikali yanayotetea kutofukuzwa shule kwa wanafunzi wasichana. Kwa mujibu wa John Magufuli kama Watanzania wangesikiliza mashirika yanayotetea haki zabinadamu kutoka nchi za Magharibi "ingelifikiia kila darasa, wanafunzi wote kuwa na watoto. Katika hali hiyo, ni nini kitakachotokea ? Wakati mwalimu anafundisha, wote wangelitoka kwenda kunyonyesha watoto zao? Kamwe katika muhula wangu wangu! ", alisem arais wa Tanzania. "Kama mashirika haya yana upendo kwa wanafunzi hawa, yangelianzisha shule maalum kwa akina mama," aliongeza rais John Pombe Magufuli.

Ripoti yashirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch iliochapishwa June 16 inasema kuwa viongozi wa shule za Tanzania walikuwa wakifanya vipimo vya mimba kwa minajili ya kufukuza wanafunzi wajawazito, na hivyo kuwanyima haki yao ya elimu.

FEMNET, shirika la haki za wanawake barani Afrika katika taarifa yake limeshtumu matamshi ya rais wa Tanzania, ambaye anataka " kuwahujumu kwa mara ya pili" wanafunzi wasicahana wanaojifungua, badala ya kushughulikia tatizo la unyanyasaji wa kijinsia katika shule.

Siku tatu tu baada ya kuchapishwa kwenye mtandao, tayari saini 100,000 zimekusanywa kufuatia maombi yaliorushwa hewani na mashrika mbalimbali. Mashirika haya yanatoa wito kwa rais Magufuli kurejelea upya kauli yake na kuweka mfumo wa kisheria kwa wanafunzi wasicahana wajawazito kuendelea na elimu yao baada ya kujifungua.

Matamshi ya Magufuli yawakasirisha wanawake Tanzania

Rais wa Tanzania John Magufuli ameshutumiwa kwa matamshi yake kwamba wasichana wanaojifungua hawafai kuruhusiwa kurudi shule, kwa mujibu wa BBC.

Ombi la mitandao ya kijamii limewekwa huku shirika moja la wanawake barani Afrika likitoa hamasa ya kumtaka rais Magufuli kuomba msamaha kwa matamshi hayo.

Bwana Magufuli aliwaonya wasichana wa shule katika mkutano wa hadhara siku ya Jumatatu kwamba ”unaposhika mimba mambo yako yamekwisha.”

Magufuli amesema kuwa chini ya uongozi wake wasichana wa shule ambao hujifungua watoto hawataruhusiwa tena kurudi shuleni.

Sheria iliopitishwa mwaka 2002 inaruhusu kutimuliwa kwa wasichana waliotungwa mimba wakiwa shuleni.

Sheria hiyo inasema kuwa wasichana wanaweza kufukuzwa shuleni kwa ”makosa yanayokiuka maadili na ndoa”.

Makundi ya haki ya wanawake yamekuwa yakiishinikiza serikali kubadilisha sheria hiyo.

Magufuli ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara katika mji wa Chalinze, takriban kilomita 100 magharibi mwa mji wa Dar es Salaam alisema kuwa kina mama hao wachanga hawatasoma vyema iwapo wataruhusiwa kurudi shule.