TANZANIA-USHOGA-JAMII

Wanaharakati wa haki za mashoga wakabiliwa na vitisho nchini Tanzania

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. REUTERS/Thomas Mukoya

Serikali ya Tanzania imetishia kuwakamata wanaharakati wa haki za mashoga na kuahidi kuwafukuza wageni ambao wataunga mkono kutetea haki za mashoga, vyombo vya tanzania viliarifu siku ya Jumatatu, Juni 26.

Matangazo ya kibiashara

"Napenda kuwakumbusha na kuonya mashirika yote na taasisi ambazo zinafanya kampeni na kudai kutetea maslahi ya mashoga (...) Tutawakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wote wanaohusika", alisema Jumapili Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba katika hotuba aliotolea umma na kurushwa na gazeti la serikali la Daily News. "Kama kuna shirika katika nchi hii ambalo linasaidia na kutetea ushoga, basi shirika hilo lipoteza usajili wake hapa," aliongeza Bw Nchemba. Waziri alionya kwamba nchi yake bila kusita itamfukuza nchini raia yoyote wa kigeni anayedai kutetea haki za mashoga.

Katika hotuba tata alioitoa siku ya Alhamisi wiki iliyopita, rais John Pombe Magufuli aliyaonya mashirika yanayotetea haki za mashoga ambayo yalitetea haki za wanafunzi wasichana wajawazito kuendelea na elimu yao baada ya kujifungua.

"Wale ambao wanafundisha mambo yasioeleweka hawatupendi, ndugu zangu. Walituleta dawa za kulevya, vitendo vya mashoga ambavyo hata ng'ombe hawawezi kufanya," rais wa Tanzania alisema.

Bw Magufuli aliwataka wananchi wake kuacha "kuiga desturi hizi za aibu", hata kama jambo hili laweza kusababisha kusimamishwa kwa misaada fulani kutoka nje. "Wao (nchi za Magharibi) wanatoa misaada, lakini misaada hii ni rasilimali zetu wanazotibia!".

Mapema mwaka huu serikali ya Tanzania ilitishia kuchapisha orodha ya mashoga wanaouza miili yao kabla ya kuachana na mpango huo baadae.

Siku chache kabla, serikali ya Tanzania iliamuru kufungwa kwa vituo maalumu vya afya vinavyopambana dhidi ya UkimwiI, baada ya kutuhumiwa kuendeleza ushoga, uamuzi uliokosolewa vikali na Marekani.

Nchini Tanzania, tendo la ushoga linaadhabiwa kwa hukumu nzito gerezani, lakini hivi karibuni serikali ilipitisha sheria dhidi ya mashoga. Ushoga umepigwa marufuku katika nchi 38 kwa jumla ya 54 za Afrika na unaadhabiwa kwa hukumu ya kifo nchini Mauritania, Sudan na Somalia, kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International.