KENYA-AL SHABAB

Mwakilishi wa serikali Pwani ya Kenya ataka msitu wa Boni kushambuliwa

Wanajeshi wa Kenya wakifanya msako katika msitu wa Boni katika Kaunti ya Lamu
Wanajeshi wa Kenya wakifanya msako katika msitu wa Boni katika Kaunti ya Lamu assets.irinnews.org

Mwakilishi wa serikali Pwani ya Kenya Nelson Marwa, anapendekeza msitu wa Boni katika Kaunti ya Lamu, unaoaminiwa kuwahifadhi magaidi wa Al Shabab ushambuliwe kwa mabomu kuwaangamiza wapiganaji hao.

Matangazo ya kibiashara

Marwa amesema msitu huo umekuwa hatari kwa sababu wanamgambo wa Al Shabab wanautumia kutekeleza mashabulizi ya kigaidi dhidi ya raia wa kawaida na maafisa wa usalama.

Hivi karibuni, mashambulizi yameendelea kuongezeka katika maeneo ya jirani ya msitu huo licha ya wanajeshi kuendeleza operesheni inayofahamika kama Linda Boni, kupambana na kundi hilo.

Soma habari zaidi. Bonyeza

Wiki hii watu nane walipoteza maisha baada ya Al Shabab kushambulia lori la maafisa wa Polisi waliokuwa wanapiga doria.

Marwa amewataka raia wanaoshi katika msitu huo kuepuka kuingia ndani yake ili kuwapa nafasi maafisa wa usalama kupambana na wanamgambo hao.