Pata taarifa kuu
KENYA-AFYA

Kenya kutumia toleo la mwisho la dawa ya mseto (DTG) dhidi ya UKIMWI

Kenya inatumia toleo la mwisho la dawa ya mseto dhidi ya Ukimwi.
Kenya inatumia toleo la mwisho la dawa ya mseto dhidi ya Ukimwi. Getty Images

Kenya ni nchi ya kwanza Afrika kutumia toleo la mwisho la dawa ya mseto dhidi ya Ukimwi. Dawa hii hboresha na huongeza maisha ya maelfu ya watu wanaosumbuliwa na ukali wa ugonjwa wa Ukimwi na kuvumilia kwa matibabu mengine.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kupasishwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani mwaka 2013, dawa ya Dolutegravir (DTG) ilitumwa kwa zaidi ya wagonjwa 20 000 nchini Kenya, kwa msaada wa UNITAID, shirika la kimataifa la uuzaji wa madawa.

UNITAID inapambana kupunguza gharama ya utengenezaji wa madawa na kuruhusu makampuni ya madawa kupata kibali cha kununu dawa hiyo kwa gharama ya chini.

Kenya, ambayo ina watu wengi wanaoishi na VVU duniani, imepiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi.

Kwa mujibu wa Sylvia Ojoo, mkurugenzi wa Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Maryland nchini Kenya anaesimamia mpango wa kuanzishwa kwa dawa ya DTG, karibu 15% ya wagonjwa wa VVU wanaonekana kuwa na nguvu , ikimaanisha kwamba madawa hayafanyi kazi kwao.

Eneo la kusini mwa Sahara lilikua, kwa miongo kadhaa, kitovu cha VVU. Eneo hili lina robo tatu ya watu walioathirika.

Hadi mwaka 2020, shirika la Umoja wa Mataifa linalopambana dhidi ya Ukimwi (UNAIDS) linatarajia kuwapa dawa za kupunguza makali ya Ukimwi karibu 90% ya watu walioambukizwa virusi vya ugonjwa huo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.