Raia wa Kenya wamchagua rais wao

Mwananchi akipiga kura kwenye uchaguzi uliopita nchini Kenya
Imehaririwa: 07/08/2017 - 22:26

Wananchi wa Kenya wanajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu siku ya Jumanne, huku hali ya utulivu ikiendelea kushuhudiwa nchini humo. Waumini wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo nchini Kenya siku ya Jumapili Agosti 6, walifurika kwa wingi kwenye nyumba za ibada, kuhudhuria misa ya mwisho ya siku ya Jumapili kabla ya uchaguzi mkuu Jumanne ya wiki ijayo.