KENYA-UCHAGUZI

Wakenya Kumchagua rais wao Jumanne

Rais Uhuru Kenya akiwa na mgombea mwenza wake William Ruto, Nakuru 5 Agosti 2017
Rais Uhuru Kenya akiwa na mgombea mwenza wake William Ruto, Nakuru 5 Agosti 2017 REUTERS/Baz Ratner

Wananchi wa Kenya wanajiandaa kwa uchaguzi mkuu siku ya Jumanne, huku hali ya utulivu ikiendelea kushuhudiwa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Waumini wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo nchini Kenya siku ya Jumapili walifurika kwa wingi kwenye nyumba za ibada, kuhudhuri misa ya mwisho ya siku ya Jumapili kabla ya uchaguzi mkuu Jumanne ya wiki ijayo.

Katika kanisa la All Saint's Cathedral la jijini Nairobi nchini Kenya, waumini walikusanyika na kufanya sala ya pamoja kuombea taifa na kuombea uchaguzi uchaguzi mkuu.

kanisa la All Saint's Cathedral la jijini Nairobi nchini Kenya.
kanisa la All Saint's Cathedral la jijini Nairobi nchini Kenya. Photo: RFI/Daniel Finnan

Kasisi mkuu wa kanisa hili Sammy Wainaina amewataka waumini kuendelea kufanya maombi kuliombea taifa, huku akiwataka vijana kutotumiwa na wanasiasa siku ya kupiga kura.

Kasisi Wainaina amesema anasikitishwa na namna ambavyo wanasiasa walishindwa kuonesha mshikamano katika kuhubiri amani ambapo badala yake walikuwa wakifanya siasa za kuwagawa raia wa Kenya kwa misingi ya ukabila.

Miaka 10 iliyopita zilishuhudiwa ghasia mbaya nchini humo, ambapo maelfu ya watu waliuawa na wengine kujeruhiwa.

Kura za maonizinaonyesha kuwepo kinyang'anyiro kikali kati ya rais wa sasa Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Mwaka 2013 Raila Odinga alidaia kuwepo udanganyifu na alipoteza kesi mahakamani.

Vinara wa muungano wa upinzani nchini Kenya, NASA, Raila Odinga na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, Nairobi, 5 Agosti 2017
Vinara wa muungano wa upinzani nchini Kenya, NASA, Raila Odinga na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, Nairobi, 5 Agosti 2017 REUTERS/Thomas Mukoya

Wakati huu, akiwa anawania kwa muhula wa nne na hasa mara ya mwisho, anaweza akaingia mitaani ikiwa atahisi kuwa kura hizo zimeibiwa.

Wiki mbili zilizopita meneja wa masuala ya kompiuta aliuawa na kisa hiki kimezua wasi wasi nchini Kenya

Chris Msando alikuwa akisimamia mifumo ya eletroniki na alionekana kwenye runinga akihakikishia umma kuwa mifumo hiyo itafanikiwa na haiwezi kudukuliwa.

Wakati mwili wakae uliokuwa na majera mabaya ulipatikana kwenye kichaka, madai yaliibuka kuwa kuna mtu alikuwa anapanga kuingilia kati uchaguzi.

Wagombea wakuu ni rais anayemaliza muda wake Uhuru Kentatta na mpinzani mkuu Raila Odinga

Bwana Kenyatta anatoka jamii ya Kikuyu na hasimu wake wa zamani William Ruto kutoka jami ya Kalenjin, walilaumiwa kwa kuchochea ghasia kati ya jamii hizo mbili.

Mashtaka yao yalihusiana na ghasia za baada ya Uchaguzi wa 2007 ambapo karibu watu 1200 waliuawa na kuwalazimu wengine maelfu kuhama makwao.