RWANDA-UCHAGUZI-SIASA

Paul Kagame atangazwa mshindi katika uchaguzi wa urais

Rais wa Rwanda Paul Kagame madarakani toka mwaka 2000.
Rais wa Rwanda Paul Kagame madarakani toka mwaka 2000. REUTERS/Eric Vidal

Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda imemtangaza rais anaye maliza muda wake, Paul kagame mshindi katika uchaguzi wa urais uliyofanyika wiki iliyopita. Paul Kagame ameibuka mshindi kwa asilimia 98.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waangalizi, kulikuwa na uhamasishaji mkubwa wa wapiga kura. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda Charles Munyaneza, zoezi la kupiga kura lilienda vizuri bila matatizo yoyote.

Kwa ushindi huu, rais wa Rwanda Paul Kagame amethibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa wiki iliopita na tume ya uchaguzi nchini humo, kwa mujibu wa shirika la habari cha AFP. Marais wengi wa Afrika wanapendelea kupata kura kama hizi ili isionekani kuwa waliiba kura.

Paul Kagame ameshinda kwa muhula wa tatu sasa wa mika saba. rais Kagame ameleta mabadiliko makubwa katika nchi yake hasa katika sekta ya uchumi, miundombinu, usalama, elimu, Afya na ustawi wa jamii, licha ya kukosolewa kwa unyanyasaji wa haki za kibinaadamu.

AFP imeripoti kwamba tume hiyo ilimuongezea rais Kagame asilimia ya kura alizopata kutoka 98.63, ikiwa ni takwimu zilizotangazwa hapo awali hadi asilimia 98.79.

Paul Kagame alipambana katika uchaguzi huo naa wapinzani wawili, na hakuna hata mmoja wao aliyepata asilimia moja ya kura