Wanafunzi 7 wafariki dunia katika mkasa wa moto Shule ya Sekondari, Nairobi
Imechapishwa:
Takribani wanafunzi saba wamefariki dunia huku wengine kumi wakijeruhiwa kufuatia moto uliozuka saa nane za usiku katika bweni la shule ya wasichana Moi mjini Nairobi,waziri wa Elimu Dr,Fred Matiang'i amethibitisha.
Akizungumza na vyombo vya habari nchini Kenya asubuhi hii waziri Matiang'i amesema bado chanzo cha moto huo hakijajulikana lakini tayari idara zote muhimu za uchunguzi zimewasili shuleni hapo kubaini chanzo cha moto huo.
Majeruhi kumi wakiwemo wawili mahututi wamekimbizwa katika hospitali ya Kenyatta mjini humo.
Aidha serikali imetoa salamu za pole na rambirambi kwa wazazi waliopoteza watoto wao katika mkasa huo ulioikumba shule hiyo na kuahidi kushirikiana nao katika kipindi hiki kigumu.
Shule hiyo imefungwa kwa majuma mawili kufuatia mkasa huo.