KENYA

Shule za bweni zamulikwa kufuatia vifo vya wanafunzi nane shule ya Moi Nairobi

Mwanafunzi wa Moi akimkumbatia mzazi baada ya wenzao kufariki kwa ajali ya moto
Mwanafunzi wa Moi akimkumbatia mzazi baada ya wenzao kufariki kwa ajali ya moto http://www.nydailynews.com

Kufuatia vifo vya wanafunzi wanane katika shule ya wasichana ya Moi jijini Nairobi hapo jana kwa ajali ya moto,kwa mara nyingine shule za bweni zimeangaziwa kwa mtazamo mkali kuhusu usalama usalama wa wanafunzi katika shule hizo.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo linakuja miezi minne baada ya kikosi kazi kilichoongozwa na serikali kupendekeza hatua kali kuchukuliwa ili kuhakikisha usalama wa wanafunzi shuleni, lakini utekelezaji wake bado hauko wazi.

Ripoti ya machafuko katika taasisi za elimu mwaka jana iliyotolewa mwezi Mei ilieleza kuwa mabweni katika shule nyingi hayana milango ya dharura ama yameziba milango ya dharura.

Takribani wanafunzi nane wamefariki dunia hapo jana huku wengine kumi wakijeruhiwa kufuatia moto uliozuka saa nane za usiku katika bweni la shule ya wasichana Moi mjini Nairobi,waziri wa Elimu Dr,Fred Matiang'i amethibitisha.