Habari RFI-Ki

Ukosefu wa ajira watajwa kuchangia ukiukwaji wa haki za watoto Tanzania

Sauti 10:07
Watoto nchini Tanzania
Watoto nchini Tanzania

Ukosefu wa ajira ni tatizo linalochangia watu kujihusisha na utekaji wa watoto ili kujipatia pesa kwa njia ya kuwatisha wazazi wa watoto hao.Hivi karibuni nchini Tanzania kumeshuhudia visa vya utekaji wa watoto ambapo watekaji wamewadai wazazi kiasi cha pesa ili kuwaachia.Kwa mujibu wa Polisi baadhi ya watekaji waliokamatwa walidai kuwa wameitumia njia hii kama mbinu ya kujipatia kipato.Watoto wawili waliotekwa wamepatikana wameuawa juma hili.