Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA-USHIRIKIANO

Majaji watatu kuchunguza benki ya BNP Paribas inayoshtumiwa katika mauaji Rwanda

Bisesero, magharibi mwa Rwanda, tarehe 2 Desemba 2015. Zaidi ya miaka 20 baada ya mauaji ya kimbari, manusura kutoka jamii ya Watutsi wanaendelea kukumbuka siku tatu za mauaji ambayo yalikumba maelfu ya ndugu zao.
Bisesero, magharibi mwa Rwanda, tarehe 2 Desemba 2015. Zaidi ya miaka 20 baada ya mauaji ya kimbari, manusura kutoka jamii ya Watutsi wanaendelea kukumbuka siku tatu za mauaji ambayo yalikumba maelfu ya ndugu zao. STEPHANIE AGLIETTI/AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Miaka ishirini na tatu baada ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda, benki ya Ufaransa inajikuta kwa mara ya kwanza katika uchunguzi wa kina kosa la kula njama.

Matangazo ya kibiashara

Majaji watatu wameteuliwa kusikia malalamiko yashirika lisilo la kiserikali ambalo linashtumu benki ya Ufaransa BNP Paribas kufadhili mwaka 1994 ununuzi wa silaha kwa manufaa ya wanamgambo wa Kihutu.

Uchunguzi huu wa mahakama ulifunguliwa Agosti 22 kwa kosa la "kula njama katika mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu," chanzo kilio karibu na kesi hii kikinukuliwa na shirika la habari la AFP kimesem Jumatatu.

Hatua hii inakuja wakati ambapo mauaji ya kimbari nchini Rwanda yanaendelea kuzua mahusiano mabaya kati ya Ufaransa na Rwanda, ambapo Rwanda inashutumu viongozi wa Ufaransa kushiriki katika mauaji hayo.

Shirika linalopambana dhidi ya rushwa la Sherpa, muungano wa vyama vya wananchi kwa Rwanda (CPCR) na shirika lisilo la kiserikali la Ibuka tawi la Ufaransa, wanashtumu benki hiikuruhusu manamo mwezi Juni mwaka 1994 "ufadhili wa ununuzi wa tani 80 za silaha "kwa manufaa ya wanamgambo wa Kihutu, wakati ambapo mauaji ya kimbari dhidi ya watu kutoka jamii ya Watutsi yalikua yakiendelea, huku vikwazo vya Umoja wa Mataifa vikikiukwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.