KENYA-MAANDAMANO-UCHAGUZI

Machafuko mapya yazuka wakati wa maandamano ya upinzani Kenya

Maandamanao ya wafausi wa muungano wa upinzani (NASA)yaliyotawanywa na polisi ikitumia gesi za machozi, Nairobi Oktoba 16, 2017.
Maandamanao ya wafausi wa muungano wa upinzani (NASA)yaliyotawanywa na polisi ikitumia gesi za machozi, Nairobi Oktoba 16, 2017. REUTERS/Thomas Mukoya

Nchini Kenya, upinzani unaendelea kuhamasisha wafuasi wake licha ya serikali kutoa hivi karibuni sheria inayopiga marufuku mikusanyiko na maandamano katika miji mikubwa mitatu.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Muungano wa upinzani NASA, Raila Odinga, ambaye alijiondoa katika uchaguzi wa Oktoba 26, amekua akiwatolea wito wafuasi wake kuandamana kila siku. Anaomba mageuzi ya Tume ya Uchaguzi na kufuta uchaguzi wa urais ambao ulipangwa kufanyika Oktoba 26. Wito huo wa kuandamana kila siku uliitikiwa siku ya Jumatatu Oktoba 16, lakini ulikabiliwa na vurugu.

Kijana mwenye umri wa miaka 18 aliuawa kwa kupigwa risasi katika mjini wa Kisumu siku ya Jumatatu, katika makabiliano kati ya waandamanaji na polisi. Mwili wa kijana huyo ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali kuu ya mji huo. Mauaji mengine yameripotiwa katika ngome ya Raila Odinga, magharibi mwa nchi, wakati ambapo mashirika mbalimbali ya kimataifa na yale kutoka Kenya yanaendelea kulaani kuongezeka kwa vurugu zinazosababishwa na polisi.

Maandamano hayo yalianza vizuri. Mamia ya waandamanaji, wakiongozwa na gavana wa Kaunti, Peter Anyang 'Nyong'o, walikusanyika mbele ya jengo la Tume ya Uchaguzi, licha ya kupigwa marufuku na serikali. Kwenye mabango waliokua wakibebelea, kulikua kumeandikwa: "Hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi". Mjini Mombasa, mji wa pili kwa ukubwa nchi Kenya, maduka mengi yalifungwa na wafuasi wa upinzani walitawanywa tena na polisi ikitumia gesi za machozi.

Hali kama hiyo ilishuhudiwa katika mji wa Nairobi, ambapo waandamanaji walikabiliana na idadi kubwa ya polisi katikati ya jiji.

Ikiwa zimesalia siku tisa kabla ya uchaguzi, serikali na upinzani wamekataa kuelewana. Kwa Uhuru upande wa Uhuru Kenyatta, amesema mikusanyiko hiyo ina lengo la kuchochea machafuko nchini, wakati ambapo Raila Odinga amewatolea wito Wakenya kudai haki yao ya kuandamana.