KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Siku mbili zasalia kujua hatma ya ushindi wa rais Kenyatta

Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta REUTERS/Thomas Mukoya

Kenya inaonekana huenda ikakwama kwa muda mrefu katika sintofahamu ya kisiasa, kikatiba na kiuchumi kufuatia mgogoro wa uchaguzi wa rais.

Matangazo ya kibiashara

Rais Uhuru Kenyatta, ambaye alishinda uchaguzi wa marudio ambao ulisusiwa na mpinzani wake mkuu Raila Odinga, anakabiliwa na muda wa siku mbili kabla ya kujua kama ataongoza kwa muhula wa pili ama atasubiri uamuzi mwingine wa Mahakama Kuu kuhusu uhakika wa ushindi wake.

Hapo jana Muungano wa upinzani NASA umezindua kampeni ya kususia bidhaa kutoka kampuni ambazo wanasema zilishirikiana na rais Uhuru Kenyatta kuiba kura.

Kampuni ambazo NASA inataka wafuasi wake na wakemya wanaopenda haki kusuisa huduma zake ni pamoja na kampuni ya Safaricom, Maziwa ya Brookside ambayo rais Uhuru Kenyatta anamiliki lakini pia bidhaa za kampuni ya Bidco.