KENYA-UCHAGUZI

Ushindi wa Uhuru Kenyatta hatarini

Wafanyakazi wa Mahakama Kuu ya Kenya wakihifadhi nyaraka za malalamiko dhidi ya uchaguzi wa urais wa Oktoba 26, 2017.
Wafanyakazi wa Mahakama Kuu ya Kenya wakihifadhi nyaraka za malalamiko dhidi ya uchaguzi wa urais wa Oktoba 26, 2017. YASUYOSHI CHIBA / AFP

Siku chache baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio nchini Kenya ambapo rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi, hatimaye ushindi huo unaonekna kuwa hatarini, baada ya baadhi ya watu kuwasilisha malalamiko yao kwa Mahakama ya Juu nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Watu wanne tayari wamewasilisha malalamiko yao kwenye Makahakama ya Juu nchini Kenya wakipinga ushindi wa Uhuru Kenyatta na kudai kuwa uchaguzi huo haukufuata sheria.

Mnamo mwezi Agosti, uchaguzi wa urais ulifutwa na Mahakama Kuu, na kupelekea uchaguzi mpya kufanyika Oktoba 26. Rais Kenyatta alichaguliwa tena. Siku ya Jumatatu, Novemba 6, wakati ambapo ilikuwa ni tarehe ya mwisho wa kuwasilisha malalamiko mahakamani kuhusu uchauzi huo, watu wanee wamewasilisha malalamiko yao kwenye Mahakama Kuu.

Mtu wa kwanza aliye wasilisha malalamiko yake ni mbunge wa zamani Harun Mwau, ambaye, amesema wakati Mahakama Kuu ilifuta uchaguzi wa Agosti 8, mchakato wa uchaguzi ungelianza upya.

Wanaharakati wawili wa haki za binadamu, Khalef Khalifa Njonjo Mue, walitoa malalamiko yao dhidi ya Tume ya Uchaguzi (IEBC) wakiishtumu kutowajibika kwa majukumu yao, upendeleo, ukiukwaji wa sheria na udanganyifu. Aidha, kwa mujibu wa wanaharakati hao, IEBC haingepaswa kuandaa uchaguzi katika mazingira ya machafuko wakati ambapo ilijua kwamba majimbo 25 hayangeliweza kushiriki kura hiyo.

Shirika linaloitwa Black Flag pia limewasilisha malalamiko yake kwenye Mahakama Kuu dhidi ya IEBC, Uhuru Kenyatta lakini pia dhidi ya Raila Odinga.

Hatimaye, shirika linalotetea Utawala wa Kidemokrasia (Institute Of Democratic Governance) limeanzisha utaratibu dhidi ya viongozi wa upinzani watano, ikiwa ni pamoja na Raila Odinga. shirika hili linawashtumu vongozi hao wa upinzani kuwasababisha vurugu za uchaguzi na kuomba wafunguliwe mashitaka.