TANZANIA-USALAMA

Watu zaidi ya sita wauawa katika mlipuko Kagera, Tanzania

wanafuzi sita wameuawa katika mlipuko wa bomu uliotokea Kagera, magharibi mwa Tanzania.
wanafuzi sita wameuawa katika mlipuko wa bomu uliotokea Kagera, magharibi mwa Tanzania. kiroyeratours

Watu zaidi ya sita ambao wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa shule ya msingi ya Kihinga katika mkoa wa Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania wamepoteza maisha kufuatia mlipuko wa kifaa kinachoarifiwa kuwa ni bomu.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashahidi, zaidi ya watu arobaini wamejeruhiwa, na wengi wamesafirishwa katika hospitali ilio karibu.

Inaarifiwa kuwa mlipuko huo ulitokea wakati wanafunzi wa shule hilo walipokua wakicheza kwenye uwanja mdogo wa mpira.

Kwa mujibu wa BBC ikinumkuu mganga mkuu wa hosipitali ya Rurenge, Dokta Maria Goreth Fredrick, wamepokea miili ya watu waliopoteza maisha na majeruhi. Baadhi ya majeruhi wako katika hali mbaya.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Agustino Olomi, amesema kwamba wanafunzi hao walikuwa wakati wa mapumziko ya saa nne, na ndipo mlipuko huo ulipotokea na kusababisha madhara makubwa ya vifo.

Jeshi la polisi tayari lipo eneo la tukio kufuatilia na kufanya uchunguzi, na taarifa kamili zitatolewa baada ya muda mfupi, chanzo cha polisi kimesema.