BURUNDI-ICC

Burundi yakataa kushirikiana na wachunguzi wa uhalifu wa kivita kutoka ICC

Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya jinai ICC
Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya jinai ICC ICC-CPI

Serikali ya Burundi imesema haitatoa ushirikiano kwa wachunguzi wa uhalifu wa kivita kutoka mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC.

Matangazo ya kibiashara

Vitendo vya uhalifu dhidi ya ubinadamu unadaiwa kufanywa na vikosi tiifu kwa serikali ya raisi Pierre Nkurunziza dhidi ya wapinzani wa kisiasa.

Mahakama iliamuru uchunguzi rasmi siku ya alhamisi juu ya uhalifu uliotekelezwa kati ya April 2015 hadi octoba 2017.

Hata hivyo wataalamu wanasema itamuwia vigumu mwendesha mashtaka wa ICC Fatou Bensouda kukusanya ushahidi pasipo kupata ushirikiano wa serikali ya Burundi ambayo mwezi uliopita ilikuwa ya kwanza kujiondoa katika mahakama hiyo yenye makao yake makuu mjini the Heague nchini Uholanzi.