KENYA-SIASA-UCHAGUZI-UHURU KENYATTA-IEBC

Hatma ya Muhula wa pili kwa rais Uhuru Kenyatta kizani

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto Ikulu jijini Nairobi
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto Ikulu jijini Nairobi Service de presse de la présidence kényane

Hatma ya rais Uhuru Kenyatta wa kenya kuhusu ikiwa atahudumu kwa muhula wa pili bado haijulikani wakati huu ambapo anahudumu kama rais wa muda kwa siku 97 hii leo tangu kumalizika kwa muhula wake wa kwanza kwa mujibu wa katiba.

Matangazo ya kibiashara

Kipindi cha kuhudumu kwake kama rais wa muda kilianza Agost August 8 na bado kinaendelea wakati mahakama ya juu nchini humo ikijiandaa kusikiliza maombi ya pingamizi dhidi ya ushindi wakkatika uchaguzi wa marudio uliofanyika October 26

Mwanasheria Mkuu Githu Muigai amekataa wito na upinzani na mashirika ya kiraia wa kuunda serikali ya mpito, akisema Katiba haielekezi kuundwa kwa serikali hiyo.

Hapo jana mmoja wa viongozi wa muungano wa upinzani nchini humo Nasa, Musalia Mudavadi ametangaza kuwa muungano huo utaitisha kura ya maoni ya kubadili Katiba ili kuhakikisha haki ya uchaguzi inatimizwa.

Mudavadi amesema muungano huo unataka kutumia nguvu ya umma kama njia ya kushinikiza mageuzi ya uchaguzi akidai kuwa chama cha Jubilee kina nia ya kutumia wingi wa wawakilishi wake bungeni na hilo ndilo wanalotaka kuzuia.