KENYA-UCHAGUZI-HAKI

Mahakama Kuu Kenya yaidhinisha ushindi wa Kenyatta

Mahakama kuu ya Kenya imetupilia mbali kesi ya Harun Mwau na wanaharakati wawili Njonjo Mue na Khelef Khalif
Mahakama kuu ya Kenya imetupilia mbali kesi ya Harun Mwau na wanaharakati wawili Njonjo Mue na Khelef Khalif REUTERS/Baz Ratner

Mahakama Kuu nchini Kenya imeamua kuwa kesi mbili zilizowasilishwa dhidi ya ucahguzi wa Oktoa 26 hazina msingi na hivyo kukubali uchaguzi wa Oktoba 26 na ushindi wa Uhuru Kenyatta.

Matangazo ya kibiashara

Jaji Maraga amesema majaji kwa kauli moja wameamua kwamba kesi zote mbili hazina msingi na kila upande utasimamia gharama zake.

Mmoja wa waliogombea urais Ekuru Aukot amesema amefurahishwa na uamuzi wa mahakama ambayo alisema imedhihirisha uhuru wake na kujitolea kwake kudumisha sheria.

Kwa upande wake , kiongozi wa wengi katika bunge la Kenya Aden Duale, amesema wananchi wa Kenya sasa wanafaa kuangazia kuungana pamoja, huku akibaini kwamba njia ni nyingi za kuendeleza umoja wao.

Mahakama imekua ikichunguza rufaa mbili zilizowasilishwa na mbunge wa zamani Harun Mwau na wanaharakati wawili wa vyama vya kiraia, Khalef Khalifa na Njonjo Mue.

Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo baada ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kususia uchaguzi huo.

Mahakama ya Juu ilikuwa imebatilisha uchaguzi wa kwanza uliokuwa umefanyika tarehe 8 Agosti ambapo Kenyatta alikuwa pia ametangazwa mshindi.

Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wakiwa nje ya jengo la Mahakama Kuui
Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wakiwa nje ya jengo la Mahakama Kuui Reuters/Baz Ratner