KENYA-UCHAGUZI

Mahakama Kuu kutoa uamuzi wake kuhusu uchaguzi wa Oktoba 26 Kenya

Mahakama Kuu ya Kenya kutoa uamuzi wake baada ya kuchunguzi rufaa dhidi ya uchaguzi wa rais, Jumatatu, Novemba 20.
Mahakama Kuu ya Kenya kutoa uamuzi wake baada ya kuchunguzi rufaa dhidi ya uchaguzi wa rais, Jumatatu, Novemba 20. REUTERS/Thomas Mukoya

Mahakama Kuu nchini Kenya inatazamia kuamua Jumatatu hii, Novemba 20 ikiwa ushindi wa Uhuru Kenyatta wa Oktoba 26 ulikua halali au la. Uamuzi mgumu ambao unakuja katika hali ya mvutano wa kisiasa inayoendelea.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama imekua ikichunguza rufaa mbili zilizowasilishwa na mbunge wa zamani Harun Mwau na wanaharakati wawili wa vyama vya kiraia, Khalef Khalifa na Njonjo Mue.

Mahakama Kuu itatoa msimamo wake kuhusu masuala kadhaa ya kisheria yaliyotolewa na walalamikaji hao. Maswali ambayo walihoji ni vurugu, vitisho na vituo vingi vya kupigia kura vilivyofungwa vinaweza kupoteza uaminifu wa uchaguzi wa Oktoba 26, huku wakiomba Tume ya Uchaguzi kuanza upya mchakato wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na uteuzi mpya wa wagombe.

Leo, Mahakama itaoa uamuzi wake kulingana na marekebisho mapya ya sheria ya uchaguzi, ambayo yalianza kutumika hivi karibuni. Kulingana na marekebisho hayo ni vigumu uchaguzi wa Oktoba 26 kufutwa. Lakini leo, uamuzi wa majaji sita unaonekana kuwa ni wa kisiasa kuliko kisheria.

Mvutano umeongezeka nchini Kenya tangu siku ya Ijumaa, Novemba 17 baada ya Raila Odinga kurejea nchini akitokea nchini Marekani. Kurejea kwake kuligubikwa na makabiliano kati ya wafuasi wa upinzani na polisi. Kuidhinisha ushindi wa Uhuru Kenyatta kutazua ghadhabu kwa wafuasi wa Raila Odinga, lakini pia kufuta uchaguzi kutaongezea zaidi mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Majaji wako katika hali ngumu ya kuchukua uamuzi. Wamekua wakikosolewa na utawala tangu uamuzi wao wa Septemba 1, na wamekataa vitisho dhidi yao. Ingawa wananchi wote wa Kenya wanasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu, uamuzi wa Jumatatu hii unaonekana kuwa utakua na bahati ndogo ya kutatua mgogoro nchini humo.