KENYA-UCHAGUZI

Kenyatta kuapishwa kwa muhula wa pili Kenya

Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto wakiwa na kibali kinachothibitisha ushindi wao baada ya matokeo ya uchaguzi yalitangazwa na Tume ya Uchaguzi Nairobi tarehe 11 Agosti 2017.
Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto wakiwa na kibali kinachothibitisha ushindi wao baada ya matokeo ya uchaguzi yalitangazwa na Tume ya Uchaguzi Nairobi tarehe 11 Agosti 2017. REUTERS/Thomas Mukoya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Somoe Ruto Kesho Jumanne wataapishwa kwa muhula wa pili na wa mwisho madarakani huku ulinzi ukiwa umeimarishwa kuelekea sherehe hizo.

Matangazo ya kibiashara

Sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wengi wa mataifa na serikali , miongoni mwao ni waziri mkuu wa Israel Benjamin Netantahu, hatua ambayo imelazimisha kuimarishwa kwa operesheni za kiusalama ikiwemo kufungwa kwa baadhi ya barabara za miji na inakadiriwa kugharimu shilingi za Kenya milioni 250.

Mahakama imepanga kufanya maandalizi ya shughuli ya kiapo cha rais leo Jumatatu.

Rais Kenyatta atakuwa anakula kiapo katika mazingira tofauti tangu mwaka 2013, wakati ushindi wake ulipohojiwa katika Mahakama Kuu, lakini akashinda,

Kwa upande wake kinara wa muungano wa upinzani Nasa Raila Odinga ambaye wafuasi wake walikuwa wakishinikiza kuaopishwa kwake kesho swa na rais Kenyatta, amekataa shinikizo hilo na kusema anaheshimu taswira yake kimataifa , sheria na katiba ya Kenya.