Awamu ya nne na ya mwisho ya mazungumzo ya kisiasa nchini Burundi kujaribu kutatua mvutano wa kisiasa uliozuka mwaka 2015 baada ya rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu, yanafanyika mjini Arusha Kaskazini mwa nchi ya Tanzania. Wawakilishi wa serikali na mashirika ya kiraia yanayoungwa mkono na serikali ya Bujumbura yanashiriki lakini wanasiasa wa upinzani chini ya umoja unaofahamika kama CNARED, wamesusia mazungumzo hayo kwa sababu mbalimbali ikiwemo suala la suala. Wanasiasa hao wanaishi nje ya nchi, wanataka mazungumzo hayo kuahirishwa. Nini hatima ya mazungumzo haya ?