BURUNDI-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

Serikali ya Burundi na washirika wake wataka mazungumzo kuhamishwa Burundi

Visa vya watu kutoweka vinaendelea kuripotiwa nchini Burundi.
Visa vya watu kutoweka vinaendelea kuripotiwa nchini Burundi. REUTERS/Mike Hutchings

Mazungumzo ya kisiasa kuhusu nchi ya Burundi yameanza mjini Arusha nchini Tanzania. Lakini mpaka muungano wa upinzani Cnared umesusia mazungumzo hayo.

Matangazo ya kibiashara

Ni awamu ya nne ya mazungumzo yanayolenga kumaliza mzozo wa kisiasa uliozuka mwaka 2015 baada ya rais Piere Nkurunziza kuamua kuwania urais.

Mratibu wa mazungumzo hayo rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa amenukuliwa akisema haya ndio mazungumzo ya mwisho kabla ya mkataba kutiwa saini.

Hata hivyo, vyama vya upinzani CNRAED ambavyo viongozi wake wanaishi nje ya nchi , na ambao wamesusia mazunumzo haya yatakayonmalizika tarehe 8 mwezi Desemba wanataka mazungumo hayo kuahirishwa ili kufanyike mashauriano ya kupatikana kwa ajenda, lakini pia wanasema wanahofia usalama wao.

Vyama vya kisiasa na mashirika ya kiraia yanayounga mkono serikali yanataka mazungumzo hayo kuhamishwa nchini Burundi, hoja ambayo muungano wa vyama vya upinzani Cnared unaona kuwa ni mbinu za utawala kutaka kuwaweka mbaroni wanasiasa kutoka muungano huo na wale ambao wamekua wakikosoa utawala wa Nkurunziza