SUDAN KUSINI-USALAMA

Zaidi ya watu 60 wauawa katika mapigano kati ya makabila hasimu Sudan Kusini

Mkimbizi akiandamana na askari wa kulinda amani, karibu na kambi ya kulinda raia (POC) ya Umoja wa Mataifa mjini Juba, Oktoba 4, 2016.
Mkimbizi akiandamana na askari wa kulinda amani, karibu na kambi ya kulinda raia (POC) ya Umoja wa Mataifa mjini Juba, Oktoba 4, 2016. ALBERT GONZALEZ FARRAN / AFP

Katika vita vya hivi karibuni ambavyo vilianza mnamo Desemba 6, watu zaidi ya 60 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa, wabunge wawili wa jimbo la Western Lakes, kilomita 250 kaskazini magharibi mwa Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Wabunge hao wamemuandikia barua rais Salva Kiir wakisema wana wasiwasi na uhasama ulioibuka kati ya makabila hasimu katikati mwa nchi hiyo.

Murle na kabila hasimu la Dinka Bor wamekua wakikabiliana na kusababisha machafuko , hali ambayo mamlaka ya Sudan Kusini inaonekana imeshindwa kukomesha.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea mwaka wa 2013 na mapigano ya mara kwa mara kati ya waasi na jeshi yamesababisha vifo vya watu wengi, huku maelfu wakiyatoroka makazi yao.