SUDAN KUSINI-USALAMA

Mkuu wa majeshi aahidi kusitisha mapigano Sudan Kusini

Vita nchini Sudan Kusini vimesababisha maafa makubwa.
Vita nchini Sudan Kusini vimesababisha maafa makubwa. REUTERS/James Akena

Mkuu wa jeshi nchini la Sudan Kusini, Jenerali James Ajinga Mawut, amesema rais Salva Kiir amewaagiza wanajeshi kutojihusiha na vita dhidi ya waasi.

Matangazo ya kibiashara

Jenerali Mawit, ameongeza kuwa serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha kuwa inatekeleza ipasavyo mkataba wa amani uliotiwa saini wiki iliyopita jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Aidha, amekanusha madai ya wanajeshi wa Juba kuwavamia waasi kinyume na makubaliano ya amani.

Wakati huo huo raia wa Sudan Kusini waliokimbilia katika mataifa jirani wameomba kiongozi mkuu wa waasi Riek Machar ashirikishwe katika mchakato wa amani nchini humo.

Wamishtumu Afrika Kusini kumzuia Bw Machar kurudi nchini Sudani Kusini.

Hata hivyo taarifa za kuzuiliwa kwa kiongozi huyo wa waasi hazijathibitishwa na serikali ya Afrika Kusini.

Vita nchini Sudan Kusini vimesababisha vifo vya watu wengi na maelfu kuyahama makazi yao.