BURUNDI-DRC-UN-MAUAJI

Umoja wa Mataifa kuchunguza mauaji ya wakimbizi 39 kutoka Burundi

Umoja wa Mataifa umesema utachunguza mazingira yaliyosababisha mauaji ya wakimbizi 39 kutoka Burundi waliokuwa wamepewa hifadhi Kamanyola, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Warundi 39 waliuawa na polisi wa DRC Kamanyola, mashariki mwa DRC, kilomita 7 na mpaka na Rwanda.
Warundi 39 waliuawa na polisi wa DRC Kamanyola, mashariki mwa DRC, kilomita 7 na mpaka na Rwanda. Latifa Mouaoued/RFI
Matangazo ya kibiashara

Wakimbizi hao waliuawa mwezi Septemba mwaka uliiopita katika jimbo la Kivu Kusini, baada ya kulalamikia kuzuiwa kwa wenzao na jeshi la serikali ya DRC.

Umoja wa Mataifa umemteua Luteni Kanali Chikadibia Isaac Obiakor kutoka Nigeria kuchunguza mauaji hayo yaliyokea katika eneo la Kamanyola.

Baada ya mauaji hayo polisi ya DRC ilisema kuwa kati ya waliojeruhiwa wamo warundi 122, askari 6, polisi 3 na raia watatu wa DRC

 Wakati huo afisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani Josue Boji alisema askari walijaribu kuwatawanya wakimbizi kwa kupiga risasi hewani lakini walizidiwa baada ya wakimbizi hao kujibu mashambulizi kwa kurusha mawe.

 Makumi kwa maelfu ya raia wa Burundi walitoroka taifa hilo wakati wa ghasia za mwaka 2015 kufuatia hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu madarakani.