SUDANI KUSINI-MAZUNGUMZO-SIASA

Serikali yasusia mazungumzo ya amani Sudan Kusini

Serikali ya Sudan Kusini imesusia mazungumzo ya amani kuhu nchi hiyo yaliyokua yalitarajiwa kuanza tangu jana Jumatatu katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Wakimbizi wa ndani katika kambi ya Bentiu nchini Sudani Kusini.
Wakimbizi wa ndani katika kambi ya Bentiu nchini Sudani Kusini. REUTERS/David Lewis
Matangazo ya kibiashara

Serikali kwa mujibu wa chanzo kutoka jumuiya ya maendeleo na uchumi Igad kukwama kwa mazungumzo hayo ni mojawapo ya chanamoto zinazoenelea kuchochea machafuko nchini Sudan Kusini.

Hii ikiwa ni jitihada ya hivi karibuni kusitisha mapigano ya kiraia yaliodumu zaidi ya miaka minne mpaka kufikia sasa.

Kwa mujibu wa cha leo kwa sababu walitaka zaidi ya wajumbe watatu kuhudhuria kikao chenyewe, wakati ambapo wajumbe watatu ndio wanahitajika kutoka kila upande.

"Serikali inataka wajumbe zaidi ya watatuu wahuhudhurie lakini IGAD inaruhusu watau pekee,"

Sudan Kusini, taifa changa, limeendelea kukubwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka kadhaa sasa.

Katika miaka minne iliyopita, maelfu ya watu wameuawa katika mapigano na kiasi ya thuluthi moja ya raia nchini wameachwa bila ya makazi.