SUDANI KUSINI-MAZUNGUMZO-SIASA

IGAD yazionya pande zinazohasiamiana Sudan Kusini

Mazungumzo ya amani kuhusu Sudan Kusini yanasuasua. Hawa hapa ni wajumbe kutoa pande zinazohasimiana nchini humo.
Mazungumzo ya amani kuhusu Sudan Kusini yanasuasua. Hawa hapa ni wajumbe kutoa pande zinazohasimiana nchini humo. AFP PHOTO / Solan Gemechu

Mazungumzo ya amani kuhusu Sudan Kusini huenda yasifike popote baada ya taarifa kuwa utawala wa Juba unatishia kususia mazungumzo haya moja kwa moja ukitaka uwakilishi zaidi kwenye mazungumzo hayo.

Matangazo ya kibiashara

Kutokana na madai hayo viongozi wa IGAD waliwajia juu viongozi wa pande zinazohasimiana kuhusu hatua zozote za kutaka kukwamisha mazungumzo ya safari hii na kutishia kuchukua vikwazo dhidi yao.

Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Workineh Gebeyehu akizungumza wakati wa ufunguzi wa mazungumzo hayo, amezilaumu pande hizo kwa kutaka kukwamisha mazungumzo hayo kwa makusudi na kuapa safari hi jumuiya yao itachukua hatua kali dhidi yao.

Tayari nchi ya Marekani imeonesha kuchukizwa na namna utawala wa Juba unavyoshiriki kwenye mazungumzo haya na kuonya kuchukua hatua zaidi dhidi ya viongozi wake.

Machafuko nchini Sudan Kusini yamesababisha vifo vya watu wengi na wengine wengi kulazimika kuyahama makazi yao.