SUDANI KUSINI-UN-HAKI

Watoto zaidi ya 300 waachiwa na makundi ya waasi Sudan Kusini

Askari wa watoto katika zoezi la kupokonywa silaha, na kurejeshwa katika maisha ya kiraia Februari 10, 2015, Pibor, katika Jimbo la Jonglei, Sudani Kusini, zoezi lililosimamiwa na UNICEF.
Askari wa watoto katika zoezi la kupokonywa silaha, na kurejeshwa katika maisha ya kiraia Februari 10, 2015, Pibor, katika Jimbo la Jonglei, Sudani Kusini, zoezi lililosimamiwa na UNICEF. AFP PHOTO/Charles LOMODONG

Zaidi ya watoto 300 waliokuwa wanatumikishwa kama wanajeshi wameachiwa kutoka jimboni Yambio nchini Sudan Kusini chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuwasaidia watoto hao kurejea kwenye jamii.

Matangazo ya kibiashara

Kati ya watoto 311 walioachiwa na makundi ya waasi, 87 kati yao ni wasichana, imesema taarifa ya tume ya umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS.

Mjumbe wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini David Shearer, amesema hii ni mara ya kwanza kwa wasichana wengi zaidi kuachiwa na makundi ya waasi.

Wanaharakati wa haki za binadamu wamepongeza hatua hii na kusema kuwa watoto hao walikua hawatendewi haki kwa kutumikishwa kama wanajeshi wakati ambapo umri wao hauwaruhusu.

Tabia hii imekua sugu barani Afrika hasa katika nchi zinazokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Masharika mbalimbali ya haki za watoto yamekua yakikemea hali hii, huku yakiomba hatua kali zichukuliwe kwa kukomesha tabia hii.