SUDANI KUSINI-MAZUNGUMZO-SIASA

Salva Kiir: Nitahakikisha amani ya kudumu inapatikana Sudan Kusini

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir. REUTERS/Stringer

Mazungumzo ya amani kuhusu Sudan Kusini yameendelea kusuasua baada ya wajumbe kuvutana kuhusu sehemu ambayo wapatanishi na upande wa upinzani wanataka iongezwe kuhusu kutolewa adhabu kwa watu watakaokiuka makubaliano ya amani.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa Serikali ya rais Kiir wamethibitisha mazungumzo hayo kusuasua huku wakikiri kukubaoiana na upande wa waasi katika masuala mengi isipokuwa hatua ambazo Troika inataka zichukuliwe dhidi ya watu watakaohusika na kuvunja au kukiuka makubaliano ya kusitisha vita.

Katika hatua nyingine rais Salva Kiir amesema serikali yake iko tayari kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana nchini mwake licha ya kuendelea kuvutana na upinzani katika mazungumzo ya mjini Addis Ababa.

Hata hivyo licho ya mazungumzo haya kusuasua, wajumbe wameendelea kukutana mjini Addsi Ababa katika kusaka suluhu ya kudumu