KENYA-VYOMBO VYA HABARI

Vituo vya Citezen TV na Inooro TV vyafunguliwa Kenya

Vituo vya runinga vya Citizen TV na Inooro Tv vimeruhusiwa kurusha matangazo yao nchini Kenya, wiki moja baada ya mitambo yao kuzimwa na serikali.
Vituo vya runinga vya Citizen TV na Inooro Tv vimeruhusiwa kurusha matangazo yao nchini Kenya, wiki moja baada ya mitambo yao kuzimwa na serikali. twitter.com/citizentvkenya

Vituo vya runinga vya Citizen TV na Inooro Tv vimefunguliwa tena nchini Kenya baada ya kufungiwa kwa zaidi ya wiki moja.

Matangazo ya kibiashara

Vituo hivi viwili ndivyo vilivyokuwa vimesalia kurejeshwa hewani, baada ya KTN News na NTV kufunguliwa mapema wiki hii.

Serikali ilizima mitambo ya runinga hizo wiki iliyopita, baada ya kudai kuwa vilikuwa vimepanga kuonesha moja kwa moja kuapishwa kwa kiogozi wa muungano wa upinzani NASA, kama rais wa wananchi.

Mashirika ya kiraia, yale ya kutetea haki za binadamu na raia wa Kenya wamelaani serikali kwa hatua hii, katika kile kinachoonekana kuwa, ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya Habari nchini Kenya.

Mahakama Kuu jijini Nairobi, iliagiza serikali kuwasha mitambo ya Televisheni tatu zilizozuiwa baada ya kudaiwa  kuwa na mpango wa kupeperusha moja kwa moja zoezi la kuapishwa kwa kiongozi wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga, kuwa rais wa watu.