TANZANIA-UNHCR-WAKIMBIZI-HAKI

Tanzania kujiondoa kwenye mpango wa kupokea wakimbizi

Wakimbizi wa Burundi wanasubiri kwenye lango la kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kaskazini mwa Tanzania tarehe 11 Juni 2015.
Wakimbizi wa Burundi wanasubiri kwenye lango la kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kaskazini mwa Tanzania tarehe 11 Juni 2015. AFP PHOTO/STEPHANIE AGLIETTI

Tanzania imetangaza kujiondoa kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa ambao husaidia wakimbizi kujenga maisha mapya katika nchi wanakoishi.

Matangazo ya kibiashara

Tanzania kwa muda mrefu imeonekana kuwa ni nchi inayaowapa hifadhi wakimbizi wengi kutoka nchi jirani.

Tanzania inawapoa hifadhi zaidi ya wakimbizi 350,000 ambao wamekimbia migogoro nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hivi karibuni Rais John Magufuli alisema kuwa kwa ajili ya usalama na sababu za kifedha, nchi yake itajiondoa kutoka kwa mfumo wa jumla wa Umoja wa Mataifa unaosaidi wakimbizi, kwa mujibu wa BBC Afrique.

Mwaka jana, Tanzania ilisimamisha usajili wa wakimbizi kwa muda mfupi na iliwahimiza wakimbizi wa Burundi kurudi nyumbani, hatua ambayo ilishtumiwa makundi mbalimbali ya wanaharakati wa haki za binadamu.

Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limebaini kwamba linatumaujumbe wa ngazi ya juu kwa ajili ya mazungumzo na serikali ya Tanzania.

Hayo yanajiri wakati ambapo katika nchi jirani ya Rwanda serikali imeanza zoezi la kusajili upya wakimbizi kutoka Burundi miaka tatu tangu wakimbilie nchi humo.

Usajili huo unafanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa, vifaa maalum vikinasa alama za macho na vidole. Mwishowe kila mmoja atapatiwa kitambulisho cha kielectroniki chenye data zinazomhusu yeye na watu wa familia yake.